Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2022

Makundi 6 Ya Watu Walioko Hatarini Kupata Homa Ya Ini A (HAV)

  HOMA YA INI AINA A, ISABABISHWAYO NA HEPATITIS A Homa hii inasababishwa na kirusi aitwae HEPATITIS A VIRUS (HAV),kumbukeni binadamu ndo kiumbe pekee ambae anaweza kubeba huyu kirusi mwilini wake (ONLY KNOWN RESORVOIR). kwa kawaida ugonjwa hauna madhara yeyote na huisha kabisa bila ya kuacha madhara ya kudumu.kiepidemiolojia ugonjwa huu upo kila sehemu duniani na kila mtu anaweza kuupata na unaweza kutokea kama mlipuko(epidemic) au kimakundi makundi(sporadic).  NAMNA YA KUUPATA HUU UGONJWA Njia pekee inayojulikana katika kuambukizwa maambukizi haya ni KUPITIA KULA AU KUNYWA CHAKULA,MATUNDA,MBOGA ZA MAJANI AU MAJI YENYE HUYU KIRUSI.Vile vile mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto alieko tumboni ila hii ni mara chache sana kutokea.  MAKUNDI YALIYO HATARI KUPATA HAYA MAAMBUKIZI 1) Wanaokula vyakula, matunda ambavo vipo katika mazingira ya uchafu. 2) Wanaokula mboga, samaki ambazo hazijaiva vizuri. 3) WAFUNGWA. 4) WAKIMBIZI 5) WANAJESHI 6) DAY CARE CENTERS DALILI ZAKE Mara...

Kiungulia kwa Mama Mjamzito.

  Kiungulia ni tatizo linalosumbua idadi kubwa ya wanawake wakati wa ujauzito. Tatizo hili hutojikeza kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito kwa baadhi ya wanawake. Kiungulia husababishwa na asidi (tindikali) kumwagika kwenye koo la chakula kutoka kwenye tumbo la chakula. Kuna sababu nyingi zinazofanya Wajawazito kupata kiungulia mara kwa mara kuliko wanawake ambao sio wajawazito. Sababu hizo ni pamoja na Mabadiliko ya homoni yanayojitokeza wakati wa ujauzito pia mfuko wa uzazi kusukuma tumbo la chakula husababisha asidi kurudi kwenye koo la chakula Nini ufanye kuondoa au kupunguza kiungulia Tazama unachokula vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni. Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips. Kula Mara nyingi kidogo kidogo  badala ya kula milo mikubwa mitatu katika siku Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka  usijipinde, itasa...

Jinsi Homa Ya Ini/Hepatitis Inavyomaliza Watu Wengi Bila Kujua.

  Si ajabu kuona leo neno Homa ya ini na likawa jina geni kwako, hii ni kutokana na kutofahamika kwa wengi duniani na kwa watanzia kwa ujumla. Na hapo ndo ukija kujua unatamani ungelijua toka zamani, lakini kwa kua umeliona leo hujachelewa bado. Homa ya Ini ni ugonjwa usababishwao na virusi aina ya Hepatitis ambao husababisha mchochota wa ini na kufanya ini kupungua utendaji kazi wake hivyo kuleta kifo ama kansa ya ini. Ugonjwa huu haujulikani na watu wengi na wengi wanaojua inawezekana alikua na ndugu yake aliepata changamoto hii au basi ni mchangia damu alipa elimu kutoka huko. Ugonjwa huu hauna dalili za moja kwa moja na umepewa ubatizo wa jina la “Silent Killer Disease” ya kwamba ni rahisi mno ukawa na homa ya ini na usijue chochote mpka pale kinga ya mwili ikizidiwa sana na kisha kuanza kuona mabadiliko makubwa na mwili kuanza kuuma bila mpangilio wowote, mara nyingi wagonjwa wa homa ya ini hulalamika kusikia maumivu ya tumbo, mwili kuishiwa nguvu, kukosa hamu ya kula, maumivu...

Signs You Have Hepatitis: What To Look Out For

  Hepatitis is an inflammatory condition of the liver caused by several different viruses. Hepatitis A, B, and C are all viral forms of the disease, with their unique symptoms. While acute hepatitis may go away on its own after a few weeks or months, chronic hepatitis can last for years and even lead to liver failure or cancer. If you think you might have contracted one of these viruses, there are a few signs to look out for. Let’s take a closer look at what each virus does to your body and how to prevent them from spreading further... There are a number of signs that you can look out for if you think you might have hepatitis. These include: One of the most obvious signs that someone has hepatitis is jaundice, which is a yellowing of the skin and eyes caused by an increase in the production of bilirubin in the liver. This can be caused by both viral and non-viral forms of the disease, although viral hepatitis is the most common. Other symptoms that could indicate a viral infection...