Kiungulia ni tatizo linalosumbua idadi kubwa ya wanawake wakati wa ujauzito. Tatizo hili hutojikeza kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito kwa baadhi ya wanawake.
Kuna sababu nyingi zinazofanya Wajawazito kupata kiungulia mara kwa mara kuliko wanawake ambao sio wajawazito. Sababu hizo ni pamoja na Mabadiliko ya homoni yanayojitokeza wakati wa ujauzito pia mfuko wa uzazi kusukuma tumbo la chakula husababisha asidi kurudi kwenye koo la chakula
Tazama unachokula
vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni.
Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai
nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips.
Kula Mara nyingi kidogo kidogo badala ya kula
milo mikubwa mitatu katika siku
Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka usijipinde, itasaidia chakula kuteremka vizuri tumboni.
Masaa matatu kuelekea kulala usile chakula. Unapolala
yatakiwa kuwe hakuna chakula tumboni itakusaidia kukontroo kiungulia .
Usivute Sigara: Kemikali zilizopo kwenye sigara
zinafanya kulegea kwa valve zinazouzia chakula kutoka.
Unapolala hakikisha unaweka mto: Hakikisha unapoenda
kulala eneo la juu la kichwa linakuwa juu kidogo.
Vaa nguo pana zisizobana
Kunywa maji baada ya kumaliza kula na siyo
katikati ya mlo
Usitumie pombe: Pombe ni mbaya hata kwa ukuaji wa
mtoto maana hupelekea mtoto kuwa na ulemavu wa ubongo na viungo. Pombe pia
hufanya valve za kwenye koo la chakula kulegea na hivo kuruusu chakula kurudi
juu.
Muone Daktari: Hali ikiwa mbaya hakikisha unaenda
hospitali, kwa kulingana na hali yako ya ujauzito, daktari atapendekeza dawa za
kukupatia. Usimeze dawa bila kupata ushauri wa daktari maana zinaweza
kukudhuru.
Comments
Post a Comment