Skip to main content

DALILI 13 ZA MTU MWENYE HOMA YA INI (CHRONIC VIRAL HEPATITIS)

 

HATUA YA PILI YA MAAMBUKIZI YA HBV NA YA MUDA MREFU (CHRONIC HEPATITIS B HBV)


Hii ndio hatua ambayo wagonjwa wengi huanza kuonyesha dalili kubwa ama madhara makubwa yatokanayo na maambukizi ya HBV. Katika hatua hii mgonjwa anakua ameshapata madhara makubwa na ya kudumu,yaani mgonjwa anakua anaumwa kwelikweli.Ikumbukwe kuna baadhi ya watu hawaoni dalili yoyote kwa hiyo wanakuja kujishtukia wameshapata madhara makubwa kama kufeli kwa ini,magonjwa ya figo,kuharibika kwa mishipa ya damu,saratani ya ini na KIFO..
Hatua hii inajumuisha madhara yahusishayo ini lenyewe (intrahepatic manifestations) na madhara yahusuyo sehemu zingine za mwili tofauti na ini(extra hepatic manifestations), baadhi ya madhara hayo ni ugonjwa wa figo(glomerular disease) na kuharibika/kushambuliwa kwa mishipa mingi ya damu katika mwili(polyarteritis nodosa)
Baadhi ya dalili zionekanazo katika hatua hii ni :- 1) Kichefuchefu(nausea)

2)Kutapika(vomiting)

3) Kuishiwa ham ya kula(anorexia)

4)Homa(fever)

5)Manjano(jaundice)

6)Kuwashwa(pruritis)

7)kukonda sana(cachexia)

8)kuota matiti kwa wanaume(gynecomastia)

9)Kuvimba tumbo (abdominal distension)

10)Maji kujaa tumboni(ascites)

12)kutapika damu(hematemesis)

13)Kuchanganyikiwa na kupoteza fahamu

ikumbukwe kuna baadhi ya mambo ambayo yanapelekea mtu kupata dalili hizo hapo juu mapema na kali,kama mtu ni MLEVI, MTUMIA MADAWA, MWENYE HIV, KISUKARI, MAGONJWA MENGINE YA MUDA MREFU KAMA SARATANI NK, KUA UMEAMBUKIZWA VIRUSI WENGINE KAMA HCV AU HDV.Hivi vitu vikiwepo basi hali na matarajio ya mgonjwa yanakua mabaya(worse prognosis).

Comments

Popular posts from this blog

Fahamu Kuhusu Matibabu, Kinga na Makundi Maalumu Yanayostahili Kinga ya Hepatitis A.

MATIBABU YAKE (HAV).  Ugonjwa kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni, kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. Na mwisho ni kupata chanjo yake.tuzingatie pia usafi mashuleni, magerezani, makanisani, misikitini, day care ceners nk. Huu unaisha wenyewe na hauhitaji matibabu ya aina yeyote.ikitokea ukawa unahitaji dawa ni za kudhibiti dalili ulizo nazo tu (supportive treatments).  Jueni ya kwamba mgonjwa anapona kabisa ndani ya miezi 6 na anakua hana shida yeyote kama madhara ya HAV, ndo uzuri Wa kirusi hiki hua sio mbaya kama wenzake.  NAMNA YA KUJIKINGA  Njia kuu ya kujikinga na haya maambukizi ni kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni,kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. na mwisho ni kupata chanjo yake, tuzingatie pia usafi mashuleni mag...

The Interpretation of Hepatitis Viral Load Test.

What is HBV Quant.? Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test assesses the level of viral infection in the body. It measures the amount of viral DNA in the blood during the infection. Generally, this test is recommended to check the efficacy of hepatitis B treatment. Hepatitis B virus spreads mainly through body fluids or unsafe sexual intercourse. Mostly the symptoms of infection fade on their own after 4-8 weeks. However, in some cases, uncontrolled levels of HepB viral load can lead to chronic hepatitis infection and liver cirrhosis. Why is HBV Quant. done? The Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test is done: For the management of patients with chronic hepatitis B infection and currently on antiviral therapy For the diagnosis of hepatitis B for baseline values and during the course of therapy to assess the treatment response. What does HBV Quant. Measure? The Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test measures the amount of hepatitis B in a blo...

Kiungulia kwa Mama Mjamzito.

  Kiungulia ni tatizo linalosumbua idadi kubwa ya wanawake wakati wa ujauzito. Tatizo hili hutojikeza kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito kwa baadhi ya wanawake. Kiungulia husababishwa na asidi (tindikali) kumwagika kwenye koo la chakula kutoka kwenye tumbo la chakula. Kuna sababu nyingi zinazofanya Wajawazito kupata kiungulia mara kwa mara kuliko wanawake ambao sio wajawazito. Sababu hizo ni pamoja na Mabadiliko ya homoni yanayojitokeza wakati wa ujauzito pia mfuko wa uzazi kusukuma tumbo la chakula husababisha asidi kurudi kwenye koo la chakula Nini ufanye kuondoa au kupunguza kiungulia Tazama unachokula vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni. Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips. Kula Mara nyingi kidogo kidogo  badala ya kula milo mikubwa mitatu katika siku Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka  usijipinde, itasa...