HOMA YA INI AINA A, ISABABISHWAYO NA HEPATITIS A
Homa hii inasababishwa na kirusi aitwae HEPATITIS A VIRUS (HAV),kumbukeni binadamu ndo kiumbe pekee ambae anaweza kubeba huyu kirusi mwilini wake (ONLY KNOWN RESORVOIR). kwa kawaida ugonjwa hauna madhara yeyote na huisha kabisa bila ya kuacha madhara ya kudumu.kiepidemiolojia ugonjwa huu upo kila sehemu duniani na kila mtu anaweza kuupata na unaweza kutokea kama mlipuko(epidemic) au kimakundi makundi(sporadic).NAMNA YA KUUPATA HUU UGONJWA
Njia pekee inayojulikana katika kuambukizwa maambukizi haya ni KUPITIA KULA AU KUNYWA CHAKULA,MATUNDA,MBOGA ZA MAJANI AU MAJI YENYE HUYU KIRUSI.Vile vile mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto alieko tumboni ila hii ni mara chache sana kutokea.
MAKUNDI YALIYO HATARI KUPATA HAYA MAAMBUKIZI
1) Wanaokula vyakula, matunda ambavo vipo katika mazingira ya uchafu.
2) Wanaokula mboga, samaki ambazo hazijaiva vizuri.
3) WAFUNGWA.
4) WAKIMBIZI
5) WANAJESHI
6) DAY CARE CENTERS DALILI ZAKE
Mara upatapo maambukizi haya, dalili huanza kuonekana ndani ya siku 10 hadi 50, dalili hizi hua hazieleweki eleweki(dalili mchanganyiko) na inaishaga zenyewe
Mojawapo ya dalili ambazo mgonjwa anaweza kuziona ni: -
1) kichefuchefu cha ghafla
2) kutapika
3) kuishiwa hamu ya kula.
4) Homa.
5) Mwili kuchoka choka(uchovu wa mwili mzima)
6) Maumivu ya tumbo upande wa kulia chini ya mbavu.
7) Mkojo wa njano
8) Choo cheupe kama karatasi
9) Manjano(dalili hii hutokea mwishoni)
10) kuwashwa(dalili hii hutokea mwishoni)
Jambo jema kwa maambukizi haya ni kwamba mgonjwa hataishia kupata madhara makubwa ya mwili au kifo na dalili zake huanza kuisha pale tu anapoanza kupata manjano.Vilevile mtu mwenye huu ugonjwa anaweza sana kumuambukiza mtu mwingine ndani ya siku 10-50 toka aambukizwe na uwezo huu hupotea pale anapopata manjano.

Tuachie comment yako hapa chini kwa ushauri na maoni nasi tutafanyia kazi.
Comments
Post a Comment