Si ajabu kuona leo neno Homa ya ini na likawa jina geni kwako, hii ni kutokana na kutofahamika kwa wengi duniani na kwa watanzia kwa ujumla. Na hapo ndo ukija kujua unatamani ungelijua toka zamani, lakini kwa kua umeliona leo hujachelewa bado.
Homa ya Ini ni ugonjwa usababishwao na virusi aina ya Hepatitis ambao husababisha mchochota wa ini na kufanya ini kupungua utendaji kazi wake hivyo kuleta kifo ama kansa ya ini.
Ugonjwa huu haujulikani na watu wengi na wengi wanaojua inawezekana alikua na ndugu yake aliepata changamoto hii au basi ni mchangia damu alipa elimu kutoka huko.
Ugonjwa huu hauna dalili za moja kwa moja na umepewa ubatizo wa jina la “Silent Killer Disease” ya kwamba ni rahisi mno ukawa na homa ya ini na usijue chochote mpka pale kinga ya mwili ikizidiwa sana na kisha kuanza kuona mabadiliko makubwa na mwili kuanza kuuma bila mpangilio wowote, mara nyingi wagonjwa wa homa ya ini hulalamika kusikia maumivu ya tumbo, mwili kuishiwa nguvu, kukosa hamu ya kula, maumivu makali upande wa kulilia kwenye ubavu pamoja na kichefuchefu na kutapika.
Kwa dalili hizi wengi hudhania ni Malaria na hapo ndo kosa kubwa linapofanyika kwani unamfanya mtu kuanza kutumia dawa ambazo hazimsaidii na zaidi anaendelea kuingia hatarini na kuwaingiza hatarini wale wanao muuguza.
Kwa taarifa ilivyo mbaya ni kwamba hapo ndo watu wengi wanaathirika kwa kua wanaowauguza hawana uelewa juu ya kujilinda zidi ya ugonjwa huu hatari hivyo inafanya maambukizi mengi kuongezeka kutokea hapa.
Na kadri mtu mmoja anaovyokaa bila kujua habari yoyote kuhusu ugonjwa huu si alie mzima wala mgonjwa basi inafanya kila mmoja kua kwenye hatari kubwa kupatwa na janga hili, watu wengi wamewaambikiza ndugu wa karibu bila kujua na walioambukizwa wakaendelea kutokujua hivyo kufanya nao wawaambukize wengine pasipo kujua.
je, unaijua hali yako ya ini?
Ndio, inatia shaka na inakufanya ujihoji uzima wako. lakini mwanzo nimesema imekusudiwa leo kuielewa changamoto hii na ufanye maamzi leo.
Ni Nini Kifanyike?
Kata mnyororo wa maambukizi kwa kuchukua uamzi wa kwenda kupima leo na kuanza kupata chanjo mara moja ili ujilinde na uwalinde wengine, chanjo inakuondolea hofu hata ukiwa kwenye vyombo vywa usafiri vya umma unakua na amani, unakua na uhuru wa kumuuguza ndugu yako hata kama akiwa na maambukizi.
Pata chanjo, Choma Chanjo leo.
Comments
Post a Comment