Skip to main content

Hawa Hapa Maadui 3 Wakubwa wa Homa ya Ini.


Hapa swali kubwa kabisaa linaulizwa ni kitu gani mtu mwenye Homa ya ini hatakiwi kutumia? Kabla sijataja vitu hivo nawakumbusha tu kua "kua karibu na Mungu". kuna mambo mengi mnoo ya kutokufanya kama mtu unaugojwa wa ini, kiasi ambacho tukikwambia kila kitu utakata tamaa, lakini leo tunakupa mambo matatu tu yakutokufanya na hapa ni kwa maana njema ya kuilinda afya na mwonekano wa mwili wako. 

Haya sasa
1. Achana kabisaa na nyama nyekundu yaani ya mbuzi, ya ng'ombe na wanyama wa porini. wazee wa zamani nyama hawakula fresh meat, walikua wanabanika inakauka  ili kutoa maji na sumu kwenye hiyo nyama. vijana wa leo tunaweza tunajivunia kula vizuri lakini tunakula sumu nyningi sana bila kujua, acha kula nyama nyekundu.

2. Vinywaji kama vile Pombe na vitu vyenye asili ya pombe namanisha pombe yenyewe na wine, soda na energy drinks acha kabisaa 

3. Punguza kufanya tendo la ndoa. Hasa wanaume Kama umeoa punguza kwa maana ya kwamba kuna siku zingine "kichwa cha nyumba" kitoe story mpka kuna kucha😂 au basi unakua ni usiku wa injili na kusoma Quran mpka kunakucha😂

Kama hujaoa ndo basi kabisaa ACHA, si kwa maana kua nataka nikufanye mtakatifu saana isipokua wanaume wanatumia nguvu nyingi kwenye tendo hilo, hivo kuitunza nguvu hiyo kwa ajili ya mwili wako kuweza kujilinda zaidi ni vizuri. 

Singles pia kuacha hili ni kuwalinda wengine pia wasiojua wala hawana uelewa juu ya huu ugonjwa. usijifanye hujui kua unaweza kumwambukiza mtu, na ikitokea uko kwenye mahusiano basi hakikisha mwenzi wako anapata chanjo kwa haraka sana hii itakupunguzia kukaa kuwaza utamwambukiza ama lah!. 

Note: Sijasema msifanye, maana ake shemeji zangu sasa mnaweza igeuza sababu hii, ila kutokufanya nako ni bora zaidi.

Ukiamua kufanya we fanya na kisha asubuhi upate supu ya kuku na mboga za majani nyingi sana sio supu ya ng'ombe na huyo kuku awe wa kienyeji😂

Kuna mtu atasema mbona masharti mengi sasa, sisi tunaamini kua ni kwa faida yako na kila hii changamoto ni vizuri ukala na kutumia vutu vyenye alkaline kubwa kama huvijui basi tumia google kuvitafuta.

Ongeza masharti kwa ajili ya kusoma wengine.

Comments

Popular posts from this blog

DALILI 13 ZA MTU MWENYE HOMA YA INI (CHRONIC VIRAL HEPATITIS)

  HATUA YA PILI YA MAAMBUKIZI YA HBV NA YA MUDA MREFU (CHRONIC HEPATITIS B HBV) Hii ndio hatua ambayo wagonjwa wengi huanza kuonyesha dalili kubwa ama madhara makubwa yatokanayo na maambukizi ya HBV. Katika hatua hii mgonjwa anakua ameshapata madhara makubwa na ya kudumu,yaani mgonjwa anakua anaumwa kwelikweli.Ikumbukwe kuna baadhi ya watu hawaoni dalili yoyote kwa hiyo wanakuja kujishtukia wameshapata madhara makubwa kama kufeli kwa ini,magonjwa ya figo,kuharibika kwa mishipa ya damu,saratani ya ini na KIFO.. Hatua hii inajumuisha madhara yahusishayo ini lenyewe (intrahepatic manifestations) na madhara yahusuyo sehemu zingine za mwili tofauti na ini(extra hepatic manifestations), baadhi ya madhara hayo ni ugonjwa wa figo(glomerular disease) na kuharibika/kushambuliwa kwa mishipa mingi ya damu katika mwili(polyarteritis nodosa) Baadhi ya dalili zionekanazo katika hatua hii ni :- 1) Kichefuchefu(nausea) 2)Kutapika(vomiting) 3) Kuishiwa ham ya kula(anorexia) 4)Homa(fever) 5)Manjano(j...

Fahamu Kuhusu Matibabu, Kinga na Makundi Maalumu Yanayostahili Kinga ya Hepatitis A.

MATIBABU YAKE (HAV).  Ugonjwa kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni, kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. Na mwisho ni kupata chanjo yake.tuzingatie pia usafi mashuleni, magerezani, makanisani, misikitini, day care ceners nk. Huu unaisha wenyewe na hauhitaji matibabu ya aina yeyote.ikitokea ukawa unahitaji dawa ni za kudhibiti dalili ulizo nazo tu (supportive treatments).  Jueni ya kwamba mgonjwa anapona kabisa ndani ya miezi 6 na anakua hana shida yeyote kama madhara ya HAV, ndo uzuri Wa kirusi hiki hua sio mbaya kama wenzake.  NAMNA YA KUJIKINGA  Njia kuu ya kujikinga na haya maambukizi ni kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni,kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. na mwisho ni kupata chanjo yake, tuzingatie pia usafi mashuleni mag...