Pamoja na uzuri wa kazi hii na majukumu ya jeshi lolote katika nchi kua ni mhimu sana katika kuhakikisha usalama wa nchi, lakini kundi hili ni moja ya makundi sensitive kwenye ugonjwa wa hepatitis.
Kutokana na mazingira ya kazi yao kua ni mazoezi yanayotoa jasho, kupata michubuko na kuishi kwa pamoja kwa wingi inawaweka kwenye hatari ya hepatitis kuenea kwa kasi endapo tu kuna mmoja kati yao ameathirika.
Na endapo akigundurika kua na shida hii mwanajeshi huzikosa fursa nyingi mnoo kiasi ambacho anaweza kuona hamna umaana wa kua mwanajeshi kwani mda wote atahesabika kua ni mgonjwa.
HASARA ANAZOZIPATA MWANAJESHI AU ASKARI BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI
1. Hawezi kwenda kusoma course.
2. Hawezi kwenda nje ya nchi kwenye majukumu ya kikazi.
3. Hawezi kufanyishwa mazoezi makali ya kumpanua uwezo wake.
Itoshe kusema anakuwepo tu yani, anakua mwanajeshi jina tu, na kwa kua wanajeshi wengi wanapenda kazi zao na fursa walizonazo basi ikitokea kakosa hizo fursa kisaikolojia hawezi kua sawa.
Basi kama una ndugu yako mwanajeshi ni vizuri mpe hii habari, afanye uchunguzi apate kujua afya yake ya ini, kujua mapema kunasaidia sana
Basi kama una ndugu yako mwanajeshi ni vizuri mpe hii habari, afanye uchunguzi apate kujua afya yake ya ini, kujua mapema kunasaidia sana
1. Inakuondolea panic mfano wakiwa wanapima kwa ajili ya kwenda course mara ghafla aambiwe anatatizo la hepatitis kwakweli inasumbua akilini sana.
2. Lakini pia inakufanya kubadili life stlye mapema ili usiendelee kulihatarisha ini.
3. kuiepusha familia yako isipate maambukizi ya homa ya ini kwa kuipeleka kupata chanjo.
Inakufanya kutafuta utatuzi mapema kabisaa kabla ya kuathirika zaidi na unapunguza matumizi ya dawa kwa mda mrefu kwasababu unakua umewahi mapemaaa
Ndugu zetu tuwatumie hii habari wachukue chanjo ili kuepuka na hili tatizo.

Comments
Post a Comment