Skip to main content

UTAFANYA NINI UKIGUNDUA KUA MWENZI/MPENZI WAKO ANA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI?



Kwanza naanza Kwa kutoa hongera Kwa wote wanao ishi na wenzi wao wenye maambukizi.


Pili naelewa ilivyo changamoto Kwa mwanaume kumweleza mke kua anachangamoto hii, ni kutokana na wanawake wengi kujua kua kupata hepatitis inatokana na kuchepuka tu na Hali hii ni tofauti Kwa yeye mke anaweza tumia kigezo Cha wakati wa kujifungua. Lakini ukweli ni kwamba Kila mtu Yuko kwenye hatari ya kupata maambuki mpka tu uchanje.

MISINGI YA NDOA
Wakati wa kufunga ndoa Kuna kiapo japo hatuishi Kwa kiapo tunaishi Kwa Upendo. MISINGI ya ndoa ni kuvumiliana, kusameheana, kupendana, kushauriana na kulekebishana na SI kusimangana, kufukuzana, kutengana wala kuvulugana.

Kipimo Cha Imani; MAJARIBU..

Sasa inapotokea Kati yenu ana homa ya ini zingatia MISINGI ya ndoa na kipimo Cha Imani, yaani huwezi kujua unampenda kiasi Gani mpka utakapojaribiwa na kubaki kwenye Msingi wa kuvumiliana... Umenielewa ??
Ni hivi...Kama mtu amepata hii changamoto uko nae then akuambie kua anahili tatizo na uamue kumwacha basi jua kabisaa kwamba hata kama uliwahi kutamka "I love you "x1000 basi zinakua Haina maana.

kingine ni kwamba ukimkuta mwenza wako anatatizo na wewe ni mzima we mshukru Mungu tu maana hata wewe hukua na ujanja wa kulikwepa ila Mungu tu. Na pengine ukipata hii shida baada ya kujua pengine Hofu Yako ndo itakua imekupelekea kupata.

Sasa, mkishajua MWENZI wako ana tatizo basi nenda kapime Kisha Anza chanjo huku mkichukua tahadhari ya namna ya kushiriki tendo la ndoa Kwa maana ya kutumia Kinga katika kipindi Cha wewe ukiwa unapata chanjo na baada ya hapo maisha yanarudi kawaida kufurahia unganiko lenu katika nyama😊.
Hili jaribu mkilivuka Kwa kusimama nae, baada ya hapo MWENZI wako atakuheshimu mnoo na niamini Mimi kwamba atakupenda mno labda tu awe mjinga mjinga.
Asante.

Comments

Popular posts from this blog

Hawa Hapa Maadui 3 Wakubwa wa Homa ya Ini.

Hapa swali kubwa kabisaa linaulizwa ni kitu gani mtu mwenye Homa ya ini hatakiwi kutumia?  Kabla sijataja vitu hivo nawakumbusha tu kua "kua karibu na Mungu". kuna mambo mengi mnoo ya kutokufanya kama mtu unaugojwa wa ini, kiasi ambacho tukikwambia kila kitu utakata tamaa, lakini leo tunakupa mambo matatu tu yakutokufanya na hapa ni kwa maana njema ya kuilinda afya na mwonekano wa mwili wako.  Haya sasa 1. Achana kabisaa na nyama nyekundu yaani ya mbuzi, ya ng'ombe na wanyama wa porini. wazee wa zamani nyama hawakula fresh meat, walikua wanabanika inakauka  ili kutoa maji na sumu kwenye hiyo nyama. vijana wa leo tunaweza tunajivunia kula vizuri lakini tunakula sumu nyningi sana bila kujua, acha kula nyama nyekundu. 2. Vinywaji kama vile Pombe na vitu vyenye asili ya pombe namanisha pombe yenyewe na wine, soda na energy drinks acha kabisaa  3. Punguza kufanya tendo la ndoa. Hasa wanaume Kama umeoa punguza kwa maana ya kwamba kuna siku zingine "kichwa cha nyumba" ...

DALILI 13 ZA MTU MWENYE HOMA YA INI (CHRONIC VIRAL HEPATITIS)

  HATUA YA PILI YA MAAMBUKIZI YA HBV NA YA MUDA MREFU (CHRONIC HEPATITIS B HBV) Hii ndio hatua ambayo wagonjwa wengi huanza kuonyesha dalili kubwa ama madhara makubwa yatokanayo na maambukizi ya HBV. Katika hatua hii mgonjwa anakua ameshapata madhara makubwa na ya kudumu,yaani mgonjwa anakua anaumwa kwelikweli.Ikumbukwe kuna baadhi ya watu hawaoni dalili yoyote kwa hiyo wanakuja kujishtukia wameshapata madhara makubwa kama kufeli kwa ini,magonjwa ya figo,kuharibika kwa mishipa ya damu,saratani ya ini na KIFO.. Hatua hii inajumuisha madhara yahusishayo ini lenyewe (intrahepatic manifestations) na madhara yahusuyo sehemu zingine za mwili tofauti na ini(extra hepatic manifestations), baadhi ya madhara hayo ni ugonjwa wa figo(glomerular disease) na kuharibika/kushambuliwa kwa mishipa mingi ya damu katika mwili(polyarteritis nodosa) Baadhi ya dalili zionekanazo katika hatua hii ni :- 1) Kichefuchefu(nausea) 2)Kutapika(vomiting) 3) Kuishiwa ham ya kula(anorexia) 4)Homa(fever) 5)Manjano(j...

Fahamu Kuhusu Matibabu, Kinga na Makundi Maalumu Yanayostahili Kinga ya Hepatitis A.

MATIBABU YAKE (HAV).  Ugonjwa kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni, kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. Na mwisho ni kupata chanjo yake.tuzingatie pia usafi mashuleni, magerezani, makanisani, misikitini, day care ceners nk. Huu unaisha wenyewe na hauhitaji matibabu ya aina yeyote.ikitokea ukawa unahitaji dawa ni za kudhibiti dalili ulizo nazo tu (supportive treatments).  Jueni ya kwamba mgonjwa anapona kabisa ndani ya miezi 6 na anakua hana shida yeyote kama madhara ya HAV, ndo uzuri Wa kirusi hiki hua sio mbaya kama wenzake.  NAMNA YA KUJIKINGA  Njia kuu ya kujikinga na haya maambukizi ni kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni,kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. na mwisho ni kupata chanjo yake, tuzingatie pia usafi mashuleni mag...