Hii ni sitori ya hepatitis ambayo pamoja na kwamba unaweza kupuuzia kuchoma chanjo, pamoja na kwamba unaweza kukaa mda mrefu nao hadi mpka miaka 20, pamoja kwamba wakati mwingine huoni dalili kabisaa, lakini kwenye Hepatitis B kwa watu wachache sana wanaweza kufa kwa mda mfupi sana.
Sasa katika homa zote za ini, homa inayosababishwa na huyu kirusi ndo hatari kushinda wote na ndo gumzo dunia nzima kwani kirusi huyu anahusika na kutokea kwa madhara mengi na makubwa ikiwemo KIFO.Kitakwimu dunia inakadiriwa kua na watu MILIONI 248 wanaoishi na hawa virusi wa HBV na inakadiriwa pia watu wapatao 600000 HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA kutokana na madhara ya HBV kwa ini na sehemu zingine za mwili. Kwa kweli hili ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla.
Nimshukuru tu Mungu kwani kwa sasa kuna chanjo nzuri dhidi ya HBV. Chanjo hii imepunguza sana maambukizi ya HBV na kwa maana hiyo vifo na madhara mengine yatokanayo na HBV yamepungua.
Niwaambie tena maambukizi ya HBV yapo sana na watu hawajijui na huyu kirusi anaweza kukuua ndani ya saa 24!!!!(fulminant hepatitis), fulminant hepatitis huambana na kufeli kwa ini na kisha mwili kuzidiwa na sumu. Ni mbaya kuliko HIV....jihadharini sana. .
Ubaya mwingine wa huyu kirusi hua anasababisha madhara makubwa na ana hatua au nyakati mbili..
1.Hua ana hatua za awali(acute hepatitis) na .
2. Hatua za baadae/muda mrefu(chronic hepatitis), hii hatua ya muda mrefu ndo mbaya Zaidi kwani inapelekea mgonjwa kupata madhara makubwa ya ini kama ini kushindwa kufanya kazi, vivimbe kwenye ini(liver cirrhosis), saratani ya ini(hepatocellular carcinoma) na KIFO, itoshe kusema tu kua chanjo ni suruhisho la homa ya ini, kadri unavyochelewa kupata chanjo ya homa ya ini ndo unaendelea kijiweka hatarini zaidi.
Je, umechoma chanjo? unasubiri nini?
Comments
Post a Comment