Skip to main content

Posts

UTAFANYA NINI UKIGUNDUA KUA MWENZI/MPENZI WAKO ANA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI?

Kwanza naanza Kwa kutoa hongera Kwa wote wanao ishi na wenzi wao wenye maambukizi. Pili naelewa ilivyo changamoto Kwa mwanaume kumweleza mke kua anachangamoto hii, ni kutokana na wanawake wengi kujua kua kupata hepatitis inatokana na kuchepuka tu na Hali hii ni tofauti Kwa yeye mke anaweza tumia kigezo Cha wakati wa kujifungua. Lakini ukweli ni kwamba Kila mtu Yuko kwenye hatari ya kupata maambuki mpka tu uchanje. MISINGI YA NDOA Wakati wa kufunga ndoa Kuna kiapo japo hatuishi Kwa kiapo tunaishi Kwa Upendo. MISINGI ya ndoa ni kuvumiliana, kusameheana, kupendana, kushauriana na kulekebishana na SI kusimangana, kufukuzana, kutengana wala kuvulugana. Kipimo Cha Imani; MAJARIBU.. Sasa inapotokea Kati yenu ana homa ya ini zingatia MISINGI ya ndoa na kipimo Cha Imani, yaani huwezi kujua unampenda kiasi Gani mpka utakapojaribiwa na kubaki kwenye Msingi wa kuvumiliana... Umenielewa ?? Ni hivi...Kama mtu amepata hii changamoto uko nae then akuambie kua anahili tatizo na uamue kumwacha basi jua ...

Jinsi Wanajeshi/Askari Wanavyoambukizwa Homa ya Ini.

  Pamoja na uzuri wa kazi hii na majukumu ya jeshi lolote katika nchi kua ni mhimu sana katika kuhakikisha usalama wa nchi, lakini kundi hili ni moja ya makundi sensitive kwenye ugonjwa wa hepatitis. Kutokana na mazingira ya kazi yao kua ni mazoezi yanayotoa jasho, kupata michubuko na kuishi kwa pamoja kwa wingi inawaweka kwenye hatari ya hepatitis kuenea kwa kasi endapo tu kuna mmoja kati yao ameathirika. Na endapo akigundurika kua na shida hii mwanajeshi huzikosa fursa nyingi mnoo kiasi ambacho anaweza kuona hamna umaana wa kua mwanajeshi kwani mda wote atahesabika kua ni mgonjwa. HASARA ANAZOZIPATA MWANAJESHI AU ASKARI BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI 1. Hawezi kwenda kusoma course. 2. Hawezi kwenda nje ya nchi kwenye majukumu ya kikazi. 3. Hawezi kufanyishwa mazoezi makali ya kumpanua uwezo wake.   Itoshe kusema anakuwepo tu yani, anakua mwanajeshi jina tu, na kwa kua wanajeshi wengi wanapenda kazi zao na fursa walizonazo basi ikitokea kakosa hizo fursa kisai...

Fahamu Kuhusu Matibabu, Kinga na Makundi Maalumu Yanayostahili Kinga ya Hepatitis A.

MATIBABU YAKE (HAV).  Ugonjwa kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni, kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. Na mwisho ni kupata chanjo yake.tuzingatie pia usafi mashuleni, magerezani, makanisani, misikitini, day care ceners nk. Huu unaisha wenyewe na hauhitaji matibabu ya aina yeyote.ikitokea ukawa unahitaji dawa ni za kudhibiti dalili ulizo nazo tu (supportive treatments).  Jueni ya kwamba mgonjwa anapona kabisa ndani ya miezi 6 na anakua hana shida yeyote kama madhara ya HAV, ndo uzuri Wa kirusi hiki hua sio mbaya kama wenzake.  NAMNA YA KUJIKINGA  Njia kuu ya kujikinga na haya maambukizi ni kufuata njia bora za usafi kwa kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni,kuosha mboga na matunda kabla ya kuyatumia, kupika vizuri mboga za majani na vyakula vingine kama samaki nk. na mwisho ni kupata chanjo yake, tuzingatie pia usafi mashuleni mag...

The Interpretation of Hepatitis Viral Load Test.

What is HBV Quant.? Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test assesses the level of viral infection in the body. It measures the amount of viral DNA in the blood during the infection. Generally, this test is recommended to check the efficacy of hepatitis B treatment. Hepatitis B virus spreads mainly through body fluids or unsafe sexual intercourse. Mostly the symptoms of infection fade on their own after 4-8 weeks. However, in some cases, uncontrolled levels of HepB viral load can lead to chronic hepatitis infection and liver cirrhosis. Why is HBV Quant. done? The Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test is done: For the management of patients with chronic hepatitis B infection and currently on antiviral therapy For the diagnosis of hepatitis B for baseline values and during the course of therapy to assess the treatment response. What does HBV Quant. Measure? The Hepatitis B Virus - Viral Load, Quantitative test measures the amount of hepatitis B in a blo...

Makundi 6 Ya Watu Walioko Hatarini Kupata Homa Ya Ini A (HAV)

  HOMA YA INI AINA A, ISABABISHWAYO NA HEPATITIS A Homa hii inasababishwa na kirusi aitwae HEPATITIS A VIRUS (HAV),kumbukeni binadamu ndo kiumbe pekee ambae anaweza kubeba huyu kirusi mwilini wake (ONLY KNOWN RESORVOIR). kwa kawaida ugonjwa hauna madhara yeyote na huisha kabisa bila ya kuacha madhara ya kudumu.kiepidemiolojia ugonjwa huu upo kila sehemu duniani na kila mtu anaweza kuupata na unaweza kutokea kama mlipuko(epidemic) au kimakundi makundi(sporadic).  NAMNA YA KUUPATA HUU UGONJWA Njia pekee inayojulikana katika kuambukizwa maambukizi haya ni KUPITIA KULA AU KUNYWA CHAKULA,MATUNDA,MBOGA ZA MAJANI AU MAJI YENYE HUYU KIRUSI.Vile vile mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto alieko tumboni ila hii ni mara chache sana kutokea.  MAKUNDI YALIYO HATARI KUPATA HAYA MAAMBUKIZI 1) Wanaokula vyakula, matunda ambavo vipo katika mazingira ya uchafu. 2) Wanaokula mboga, samaki ambazo hazijaiva vizuri. 3) WAFUNGWA. 4) WAKIMBIZI 5) WANAJESHI 6) DAY CARE CENTERS DALILI ZAKE Mara...

Kiungulia kwa Mama Mjamzito.

  Kiungulia ni tatizo linalosumbua idadi kubwa ya wanawake wakati wa ujauzito. Tatizo hili hutojikeza kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito kwa baadhi ya wanawake. Kiungulia husababishwa na asidi (tindikali) kumwagika kwenye koo la chakula kutoka kwenye tumbo la chakula. Kuna sababu nyingi zinazofanya Wajawazito kupata kiungulia mara kwa mara kuliko wanawake ambao sio wajawazito. Sababu hizo ni pamoja na Mabadiliko ya homoni yanayojitokeza wakati wa ujauzito pia mfuko wa uzazi kusukuma tumbo la chakula husababisha asidi kurudi kwenye koo la chakula Nini ufanye kuondoa au kupunguza kiungulia Tazama unachokula vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni. Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips. Kula Mara nyingi kidogo kidogo  badala ya kula milo mikubwa mitatu katika siku Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka  usijipinde, itasa...

Jinsi Homa Ya Ini/Hepatitis Inavyomaliza Watu Wengi Bila Kujua.

  Si ajabu kuona leo neno Homa ya ini na likawa jina geni kwako, hii ni kutokana na kutofahamika kwa wengi duniani na kwa watanzia kwa ujumla. Na hapo ndo ukija kujua unatamani ungelijua toka zamani, lakini kwa kua umeliona leo hujachelewa bado. Homa ya Ini ni ugonjwa usababishwao na virusi aina ya Hepatitis ambao husababisha mchochota wa ini na kufanya ini kupungua utendaji kazi wake hivyo kuleta kifo ama kansa ya ini. Ugonjwa huu haujulikani na watu wengi na wengi wanaojua inawezekana alikua na ndugu yake aliepata changamoto hii au basi ni mchangia damu alipa elimu kutoka huko. Ugonjwa huu hauna dalili za moja kwa moja na umepewa ubatizo wa jina la “Silent Killer Disease” ya kwamba ni rahisi mno ukawa na homa ya ini na usijue chochote mpka pale kinga ya mwili ikizidiwa sana na kisha kuanza kuona mabadiliko makubwa na mwili kuanza kuuma bila mpangilio wowote, mara nyingi wagonjwa wa homa ya ini hulalamika kusikia maumivu ya tumbo, mwili kuishiwa nguvu, kukosa hamu ya kula, maumivu...